Sanaa ya watu wa Asili: Muunganisho wa Nchi na dirisha kwa siku za nyuma

Lead Image.jpg

Gamilaraay/Bigambul and Yorta Yorta artist Arkeria Rose Armstrong Credit: Arkeria Rose

Kukumbatia mila zao zaku simulia hadhithi, watu waki Aboriginal na wanavisia wa Torres Strait wame tumia sanaa kama mbinu yaku changia hadithi za utamaduni wao, imani za kiroho na maarifa muhimu ya ardhi.


Key Points
  • First Nation’s artwork is diverse and is not limited to dot painting.
  • Art was one medium in which cultural stories, spiritual beliefs and knowledge were passed down generations, and is continued today.
  • These artworks help artists feel connected to their Country.
  • Symbols are up to the interpretations of the artists using them.
Kazi za sanaa za Mataifa ya Kwanza, ni miongoni mwa kazi kongwe zaidi duniani na zina utajiri wa historia, kwa mfano ambayo ina kadiriwa kuwa na miaka 17,500.

Kazi hizi za sanaa zime hudumu kama mbinu muhimu ambazo wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait, wametumia kuendelea kuchangia hadithi zao zakitamaduni, imani zao za kiroho pamoja na ujuzi muhimu wa ardhi.

Sanaa ya watu wa asili ina utajiri unao jumuisha anuai ya mitindo na mbinu, yenye chimbuko kwa nchi za watu wa mataifa ya kwanza, tamaduni na jamii.

Hata hivyo, watu mara nyingi huwa na dhana potofu kuhusu Sanaa yawa Aboriginal ame elezea Maria Watson-Trudgett, mwanamke wa ukoo wa Koori na ‘maji safi’ wa watu wa Wiradyuri.

Bi Watson-Trudgett ni mshauri kutoka jumuiya ya Mataifa ya Kwanza, alijifunza mwenyewe pia kuwa msanii ambaye ana shauku yakuchangia tamaduni yake yaki Aboriginal.
MWT with artworks.JPG
Maria Watson-Trudgett is a First Nations consultant, a self-taught artist, and a storyteller Credit: Maria Watson-Trudgett Credit: Courtesy of Richmond Fellowship Queensland, 2019
“Baadhi ya watu wana dhana walizo jipa kuwa michoro ya nukta niya kitamaduni na aina ya kweli pekee ya sanaa yaki Aboriginal. Ila sivyo na, ni fikra zisizo sahihi.

“Sanaa yetu yakitamaduni ilihusu zaidi kuweka alama kwa kutambua vifaa, kufanya michoro katika miti wakati wa sherehe na katika sehemu zaku zika au, kupaka mwili rangi kwa sababu za sherehe. Haikuwa sana,” ame elezea.

Bi Watson-Trudgett ame ongezea kuwa michoro ya nukta ili ibuka katika miaka ya 1970 kupitia , jamii ndogo yaki Aboriginal inayo patikana katika eneo la kaskazini magharibi ya Alice Springs. Ni hapa ndipo wasanii waki Aboriginal walianza kutambulisha hadithi zao zakitamaduni kwa kutumia aina fulani ya rangi za akriliki kwenye bodi.
There are many styles of Aboriginal art that artists use to convey their stories and their cultures. Aboriginal art is anything an Aboriginal person paints that connects them to their Country and culture, and creates... a sense connection and belonging [for them].
Maria Watson-Trudgett

Kuchangia Utamaduni

Bi Watson-Trudgett alianza kufanya sanaa mnamo mwaka wa 2009 kama njia yakupumzika kutoka kwa mafadhaiko ya masomo ya chuo. Hata hivyo, alikuja kugundua kuwa sanaa ilitoa fursa nyingi zaidi “yakutuliza ubongo”.
It’s about sharing my story with other people, [and] keeping my culture alive. It also supports me connect to my Aboriginal culture, to my Country, to my old my people, and to the knowledge that I learnt while growing up on Country with family.
Maria Watson-Trudgett
Arkeria Rose Armstrong, ni msanii kutoka jumuia yawatu wa Gamilaraay/Bigambul na Yorta Yorta, anakumbuka kwa furaha hadithi zilizo changiwa nama babu zake.

Bibi yake, alikuwa kiongozi katika jamii yawa Gamilaraay, alikuwa mmoja wa wasanii wa mwisho walio kuwa wakitumia mchanga kutengeneza sanaa kandani.

“Alikuwa aki elezea hadithi zake wakati anaketi chini, kwenye nchi, kwenye nchi ya mchanga na ange tuambia hadithi katika mchanga,” ame elezea.

Hadithi hizi, zilizo changiwa kupitia vizazi, zinajumuisha hadithi zaku umba, wanyama, nyota na uzoefu wa bibi yake aki kuwia katika nchi yake. Kila hadithi ilikuwa na mafunzo yake binafsi, amesema.
IMG_0580.jpg
Art has always been part of Arkeria Rose Armstrong’s life. Credit Arkeria Rose Armstrong
“Ali elezea safari yake na hadithi zake kupitia kazi za sanaa. Kwa hiyo, kulikuwa na ishara na taswira nyingi ambazo ange tueleza zilichangiwa hivyo.”

Bi Armstrong ame elezea sanaa yake kama "kuingiliana kwa nchi zake mbili.”

Amesema huwa ana pata motisha kutoka ishara na picha alizo pata kutoka kwa bibi yake, wakati mbinu zake zime shawishiwa na babu yake ambaye ni msanii pia.

Kuelezea tena hadithi kupitia kazi zake binafsi za sanaa, huruhusu Bi Armstrong kutathmini mahusiano yanayo unga hadithi hiyo, na kuibua hisia nyingi—anazo changia na binti yake pia.
To continue culture, you need to share culture, and you need to practice culture. To share with our next generation is to make sure that they’re always at the table having those conversations.
Arkeria Rose Armstrong

Kuungwa kwa Utamaduni

Davinder Hart ni msanii mwenye familia yake ina chimbuko kutoka kanda ya kusini magharibi ya Nchi ya Noongar, Magharibi Australia. Katika utoto wake alikuwia Adelaide, kabla yaku ungwa na jumuiya yake katika Nchi ya Ngemba, jimboni New South Wales, baadae katika maisha yake.

Bw Hart alipitia uzoefu wa changamoto nyingi wakati wa miaka yake ya mapema, aliondoka shuleni akiwa na umri wa miaka 16, alipata wakati mgumu kupata kazi pamoja na kukabiliana na matumizi ya mihadarati.

Hata hivyo, msaada na mwongozo kutoka kwa wajomba na kaka zake ulikuwa muhimu, kumsaidia kubadilisha maisha yake naku ungwa tena na tamaduni yake, ambayo mara nyingi humulikwa katika kazi zake za sanaa.

“Nilikuwa na bahati kukutana na wajomba na kaka zangu, ambao walinifunza hadithi kuhusu Nchi, na hadithi hizo zinakufunza jinsi yaku jiendesha katika hali chanya,” amesema.

Kwa Bw Hart, sanaa si tu njia yaku ungwa na tamaduni yake ila, ni mbinu ya uponyaji.

“Bilashaka, mimi huwa katika hali ya ustaarabu ninapo kuwa niki chora. Nadhani wakati mwingi moyo, huongoza michoro na michoro huji chora yenyewe. Ni matibabu sana,” ame elezea.
IMG_20231021_143030_105.jpg
Davinder Hart at Saudi Arabia, UN gala dinner, 2023. Credit Davinder Hart

Kuwa sehemu ya simulizi iliyo changiwa

Bi Watson-Trudgett ame elezea kuwa wasanii wa Mataifa ya Kwanza wanaweza jumuisha aina tofauti ya ishara kwa kazi zao, baadhi ambazo ni maalum kwa nchi yao, kama nyayo za wanyama.

Mistari inayo tiririka na alama zawa Aboriginal katika kazi yake,
inafanana na jinsi mababu zake walivyo wasiliana walipokuwa wakichora maonesho na alama kwenye udongo.

Wakati baadhi ya ishara zinaweza fanana, zingine zinaweza kuwa na maana tofauti kwa wasanii tofauti.

“Kuna nafasi ya ufafanuzi wa ishara kwa msanii anaye zitumia. Usiwahi fikiria kuwa ishara fulani inaweza kuwa na maana moja kwa msanii mwingine,” amesema.
Bi Armstrong amesema sehemu nzuri yakuanzia niku uliza kuhusu hadithi zinazo elezewa katika kazi zao za sanaa.

“'Yule mtu wa Mataifa ya Kwanza ni nani? Nchi hizo ni gani na wana fananaje?' Unapo anza kuuliza maswali hayo, una anza kuona nakumhisi mtu huyo,” amesema.

“Baadhi ya njia ninazo penda zaku changia kazi zangu za sanaa, nikupitia maonesho na kuwa pale, ili uweze keti chini nakuzungumza na watu kuhusu kazi ya sanaa.

“Nadhani wakati mwingine ina kikwazo chake, tunapo changia hadithi kwenye kadi ndogo, iliyo kando ya kazi ya sanaa. Kutegemea na uhusiano wa mtu binafsi ndivyo mengi yana changiwa. Kama mwanamke wa Gamilaraay, huwa tunachangia mtu anapo kuwa tayari kujifunza.”

“Kuwa wazi kabisa, usi ogope kuuliza maswali,” Bwa Hart ame ongezea.

“Na katika mazungumzo hayo, tunajenga uhusiano kupitia hilo.”

Share