Taarifa ya Habari 14 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mweka hazina Jim Chalmers amesisitiza bajeti atakayo tangaza inahusu kuweka shinikizo yakupunguza mfumuko wa bei.


Wanachama wa upinzani wana ikosoa serikali kwa kufeli kushughulikia mfumuko wa bei. Msemaji wa maswala ya fedha katika upinzani Angus Taylor, amesema ukuaji wa muda mrefu unaongozwa kwa biashara binafsi badala ya matumizi ya serikali. Aliguzia kwa $45 bilioni za matumizi ambayo upinzani wa mseto ulipinga, mfuko wa ujenzi upya wa taifa ukijumuishwa, mfuko wa nyumba pamoja na matangazo ya makato ya kodi.

Wahalifu wakubwa wa unyanyasaji wa kijinsia jimboni New South Wales, watapata wakati mgumu sana kuachiwa huru kwa dhamana, baada ya pendenekezo za sheria mpya kuafikiwa. Wahalifu wenye hatari kubwa ambao wame achiwa huru tayari kwa dhamana, wata vishwa vifaa vyaki elektroniki kufuatiliwa. Mageuzi hayo yakisheria wanatarajiwa kupitishwa ndani ya bunge la jimbo wiki hii, kuwalenga wahalifu wabaya zaidi wanao kabiliwa kwa kifungo cha miaka 14 au zaidi gerezani. Kama wewe au mtu unayejua anataka zungumza kuhusu familia au ukatili wa nyumbani, piga simu kwa namba hii 1800RESPECT au 1800 737 732 au pigia simu shirika la Lifeline kwa 13 11 14. Katika dharura pigia simu, 000.

Kamishna wa eSafety anakabiliwa na kushindwa katika vita vyake vya kisheria dhidi ya mtandao wakijamii wa X, kuhusu kuficha video ya shambulizi la kisu ndani ya kanisa la Magharibi Sydney mwezi Aprili wakati wa ibada iliyo peperushwa mtandaoni. Kamishna wa eSafety alitaka agiza la muda linalo amuru X izuie madazeni ya tovuti yenye video ya Askofu Mar Mari Emmanuel akishambuliwa hadi wakati Hakimu Geoffrey Kennett atakapo amua kama mtandao huo wakijamii uli kiuka sheria zozote. Amri imetolewa na iliongezwa Aprili ila, Hakimu Kennett alikataa ombi hilo lakuongeza muda wa agizo hilo kabla ya kikao cha mahakama kuu ya shirikisho Jumatano [[15 MEI]].

Rwanda siku ya Jumapili ilipuuzilia mbali madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha kundi la waasi linaloshutumiwa kwa milipuko ya guruneti na kujeruhi watu kadhaa, na kuzidisha uhusiano mbaya kati ya majirani hao wa Afrika Mashariki. Takriban watu 38 walijeruhiwa katika shambulio la siku ya Ijumaa mjini Bujumbura, wizara ya mambo ya ndani ya Burundi ilisema, ikitoa lawama kwa waasi wa RED-Tabara. Gitega alisema Kigali ilitoa mafunzo na msaada wa vifaa kwa waasi, ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya Burundi kutoka katika kambi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alikanusha madai hayo, akisema hayana uhusiano kabisa na shambulio hilo. Tunatoa wito kwa Burundi kutatua matatizo yake ya ndani na kutoihusisha Rwanda na mambo hayo mabaya. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili mara nyingi umekuwa wenye matatizo na Rwanda hapo awali ilikanusha madai ya kuwa inaunga mkono waasi.

Idadi ya vifo kutokana na kuanguka kwa jengo moja nchini Afrika Kusini imepanda hadi 20, mamlaka za manispaa zimesema Jumapili, huku watu 32 wakiwa bado hawajulikani waliko kwa karibu wiki moja baada ya jengo hilo kuanguka. Timu za uokoaji zimekuwa zikifanya kazi bila kuchoka tangu jengo hilo la ghorofa lililokuwa bado kwenye ujenzi kusini mwa mji wa George lilipoanguka Jumatatu mchana huku wafanyakazi 81 wakiwa kwenye eneo hilo.

Zaidi ya asilimia 90 ya shule nchini Kenya zimefunguliwa leo, baada ya kufungwa kwa takribani wiki mbili kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu 270. Kulingana na naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga, baadhi ya wanafunzi ambao shule zao zimeathirika sana, wataendelea na masomo katika shule zingine za karibu. Awali, serikali nchini humo ilipanga kufungua shule tarehe 29 mwezi uliopita baada ya likizo ya wiki tatu, lakini ililazimika kuahirisha mara mbili kutokana na uharibifu wa barabara na shule. Shule zipatazo 2,000 nchini humo, ziliathirika na mafuriko ikiwemo uharibifu huku baadhi ya familia zikikosa makazi.

Share