Taarifa ya Habari 26 Aprili 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Aliyekuwa mu Australia wa mwaka wa zamani Rosie Batty ame ihamasisha serikali ya New South Wales izingatie kuanzisha tume yakifalme kwa ukatili wa nyumbani.


Kiongozi wa New South Wales Chris Minns amezindua tathmini kwa ukatili wa nyumbani na sheria za dhamana, baada ya mwanaume mwenye miaka 28 Molly Ticehurst kushtumiwa kwa kumuuwa mpenzi wake wa zamani. Serikali ya Victoria ili kubali mapendekezo 227 ya tume yakifalme kwa unyanyasaji katika familia, ambayo tume yakifalme ilifanya mwaka jana.

Mbunge wa eneo bunge la Fowler la Magharibi Sydney, Dai Le amesema, amekuwa akizungumza na wakaaji wa Wakeley tangu kisa cha kudungwa kisu Askofu mmoja ndani ya kanisa katika eneo la magharibi Sydney April 15.

Waziri katika serikali ya Labor Bill Shorten ame mkosoa mmiliki wa kampuni ya X Elon Musk kwa tuhuma zake za udhibiti dhidi ya uamuzi wa mahakama ya shirikisho, kuficha video inayo onesha askofu mjini Sydney akidungwa kisu katika shambulizi linalo shukiwa kuwa lakigaidi. Hali hiyo imejiri wakati Askofu Mar Mari Emmanuel alitoa taarifa katika umma, baada yakudungwa kisu mara kadhaa wakati wa ibada iliyo peperushwa mubashara mtandaoni katika eneo la kusini magharibi Sydney Aprili 15, akisema hapingi video hiyo kusalia katika mitandao yakijamii kwa sababu ni "ni haki yetu tuliyo pewa na Mungu kuwa na uhuru wakujieleza." Kwa upande wake kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema amekubaliana na uamuzi wa kamishna wa e-Safety, kuondoa vitu vinavyo kera ila, amesema pia ni ujinga kwa serikali kutarajia video hiyo iondolewe kwa umma wakimataifa.

Mfalme Charles wa Uingereza ametoa idhini yake kuwa sheria mpango wa Waziri Mkuu Rishi Sunak kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda. Hili limetokea wakati jeshi la polisi nchini Uingereza likisema waliwakamata raia wa Sudan and Sudan Kusini ambao walikuwa wakiwasaidia uhamiaji haramu kuingia nchini humo. Idhini ya Kifalme ni hatua ya mwisho katika mchakato wa sheria, na kwa ufanisi kupitisha uamuzi uliochukuliwa na bunge mapema wiki hii kuidhinisha mswaada baada ya malumbano ya muda mrefu kati ya serikali na wapinzani wa mpango huo.

Jeshi la Afrika Kusini litaongeza muda wa kutumwa kwa wanajeshi wake katika nchi zilizokumbwa na mzozo Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rais Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa yake siku ya Jumatano. Kurefushwa kwa muda huo, kwa muda usiojulikana, kutawaweka wanajeshi 1,198 wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF) mashariki mwa Congo, ambako ni sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kinachoisaidia Congo kupambana na makundi ya waasi. Taarifa hiyo pia ilisema kuwa wanachama 1,495 wa SANDF wataendelea na operesheni zao nchini Msumbiji, ambapo wamekuwa wakiunga mkono mapambano ya serikali dhidi ya itikadi kali katika maeneo ya kaskazini tangu 2021.

Miili ya watu wasiopungua 13 imeopolewa kutoka maeneo tofauti ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi baada mafuriko ya kutisha kulikumba taifa hilo la Afrika Mashariki. Serikali imeunda kikosi cha dharura kushughulikia janga hilo.Wakati huohuo, idara ya polisi imeendelea na juhudi za uokozi kwa ambao nyumba zao zimefunikwa na maji.
Kulingana na idara ya polisi, miili ya watu wasipungua 13 imepatikana maeneo tofauti tofauti ya mji Nairobi kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha. Vifo 11 vimetokea eneo la Mathare, moja Kibera na nyengine mtaani Kayole. Ifahamike kuwa haya ni maeneo ya mitaa ya mabanda jijini Nairobi. Inahofiwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka japo juhudi za uokozi zinaendelea. Maelfu wameachwa bila makaazi kwani mvua hiyo imesababisha mafuriko yaliyoathiri nyumba na baadhi ya barabara sasa hazipitiki.


Share