Taarifa ya Habari 28 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri wa maswala ya kigeni wa Australia Penny Wong amesema shambulizi baya la anga la Israel katika mji wa Rafah, linatisha na halikubaliki. Takriban watu 45 wame uawa baada ya shambulizi hilo kusababisha moto mkubwa katika kambi ya mahema ya kitongoji cha Tel Al-Sultan.


Maelfu ya watu walikuwa wakipata hifadhi hapo baada ya shambulizi la Israel katika eneo la mashariki ya Rafah wiki mbili iliyo pita. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema shambulizi hilo halikuwa na lengo lakusababisha majeraha kwa raia na uchunguzi wa kina utafanywa. Seneta Wong amesema Australia inataka pawe usitishwaji wa mapigano yakibinadam sasa hivi. Ila kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt amesema Israel haijali wito wa Seneta Wong na balozi wa Israel mjini Canberra anastahili timuliwa nchini kwa ajili yakutuma ujumbe mkali zaidi.

Kampeni mpya katika lugha imezinduliwa jimboni New South Wales, kwa lengo laku ongeza uelewa kwa udhibiti wakulazimishwa. Ujumbe huo umeadaliwa kwa watu wanao zungumza lugha kama Mandarin, Kiarabu, Kivietnam na Ki cantonese. Tafsiri zaidi katika lugha zingine zinatarajiwa katika miezi ijayo na, kampeni inayo walenga watu wa mataifa ya kwanza katika wiki ijayo. Utafiti wa 2021 umepata kuwa nchini Australia mwanamke mmoja kati ya watatu ambao ni wakimbizi na wahamiaji, hupitia aina fulani ya uzoefu wa unyanyasaji wakifamilia. Supriya Singh ni profesa wa sosholojia katika chuo cha La Trobe, amesema wahamiaji haswa wako katika hali mbaya. Kuanzia Julai, jimbo la New South Wales litakuwa mamlaka ya kwanza nchini Austrlaia kuwasilisha kosa la pekee la udhibiti wa kulazimishwa. Sheria mpya za kulazimishwa, zita anza kutumiwa jimboni Queensland kuanzia mwaka ujao.

Upinzani wa shirikisho unadai takwimu mpya zina onesha kuna ongezeko la matukio ya uhalifu miongoni mwa wafungwa wa uhamiaji walio achiwa huru. Gazeti la The Sydney Morning Herald linaripoti kuwa kuna angalau watu 28 kati ya watu 153 ambayo ni takriban theluthi tano ya walio achiwa huru katika uamuzi mkubwa wa mahakama kuu Novemba mwaka jana, ambao wamefunguliwa mashtaka ya uhalifu tangu walipo achiwa huru. Haijulikani ni wangapi miongoni mwa wafungwa hao ambao wanafanyiwa ufuatiliwaji waki elektroniki. Mbunge wa upinzani David Littleproud ame eleza shirika la habari la Nine Network kuwa serikali inafeli kwa swala usalama wa jumuiya.

Matukio ya hali mbaya ya hewa yaliyolikumba bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, na dhoruba za kitropiki, mafuriko na ukame yamesababisha majanga ya njaa ukosefu wa makazi. Na kupelekea tishio jingine baya: ikiwemo milipuko mibaya ya kipindipindu barani humo. Huko Kusini na Mashariki mwa Afrika, zaidi ya watu 6,000 wamefariki na takribani visa 350,000 vimeripotiwa tangu mfululizo wa milipuko ya kipindipindu ianze mwishoni mwa mwaka 2021. Malawi na Zambia zilipata milipuko mibaya iliyovunja rekodi, Zimbabwe imekubwa na matukio kadhaa, Kenya, Ethiopia na Somalia pia zimeathiriwa vibaya.

Raia nchini Afrika Kusini waanza kupiga kura chini ya kiwingu cha kuvurugika kwa hali ya usalama haswa baada ya kituo cha kuhifadhia karatasi za kura kuvamiwa. Raia wa Afrika Kusini wapatao milioni 1.6 waliokidhi vigezo vya kupiga kura mapema wameanza kufanya hivyo leo chini ya kiwingu cha wasiwasi wa kuvurugika usalama kwenye jimbo la kwaZulu-Natal kutokana na wafuasi wa chama cha uMkhonto we Sizwe kuvamia kituo cha kuhifadhia vifaa vya kupigia kura Jumapili. Zoezi la upigaji kura maalumu limefanyika kwa amani nchini kote kwani hakuna kitendo cha uvunjifu wa usalama kilichoweza kuripotiwa.

Baadhi ya makampuni ya usafirishaji nchini Tanzania yametangaza ongezeko la gharama za usafirishaji wa mizigo kutoka China na Dubai hadi Dar es Salaam. Hali inayoleta wasiwasi wa kuongezeka kwa gharama za maisha kwa wananchi wa kipato cha chini.
Kufuatia hatua hiyo, baadhi ya Wachumi nchini humo wameitaka serikali kubuni sera ya kuchochea uzalishaji wa bidhaa muhimu ndani ya nchi ili kupunguza uagizaji wa nje, na kusaidia kuepusha ongezeko la bei kwa bidhaa pindi inapotokea changamoto katika mnyororo wa usambazaji.

Share