Taarifa ya Habari 29 April 2024

City - Swahili.jpg

Mratibu wa maandamano yakupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake mjini Canberra, amesema waziri mkuu alidanganya kuhusu, kuto ruhusiwa kuzungumza katika tukio hilo.


Anthony Albanese ali eleza waandamanaji jumapili 28 Aprili kuwa yeye, pamoja na waziri wa wanawake Katy Gallagher, walikuwa wameomba kuzungumza katika tukio hilo ila hawaku ruhusiwa na waandalizi wa tukio hilo. Video za tukio hilo zinaonesha Sarah Williams, mmoja wa waratibu wa tukio hilo, akisimama kando ya Bw Albanese akisema huo ni uongo, kabla yaku anza kulia. Baadae Jumapili, alichapisha taarifa katika mtandao wa jamii kwa mara nyingine akisema, ali danganya nakuamua ghafla kuzungumza kwa sababu alikuwa akizomewa.

Mamlaka ya kamisha wa eSafety yanaweza ongezwa, wakati serikali inatangaza (leo jumatatau 29) kuwa itafanya tathmini ya sheria ya usalama mtandaoni. Waziri wa Mawasiliano Michelle Rowland amesema serikali inatafuta maoni ya umma kwa sheria hiyo, ambayo ina chunguzwa kwa uhuru na mwenyekiti wa zamani wa ACCC Delia Rickard. Lengo la muswada huo unalengo laku hakikisha usalama wa, wa Australia dhidi ya madhara mtandaoni, na tathmini hiyo inazingatia jinsi yakujibu hotuba ya chuki pamoja na kuzalisha kwa akili ya bandia. ((Tangazo hilo limefuata mjadala mkali kuhusu usalama wa mtandaoni, baada ya video zaku kera pamoja na taarifa potofu kuchangiwa mtandaoni baada ya mashambulizi mawili ya visu mjini Sydney mapema mwezi huu.
Kamishna wa eSafety amezindua vita vyakisheria dhidi ya kampuni ya X, baada ya mtandao huo wakijamii kukataa kufuata amri zaku ondoa video hiyo mtandaoni.

Nchini Ujerumani, kesi dhidi ya wanaume tisa ambao wame shutumiwa kwa uhaini, jaribio laku uwa na kupanga mabadiliko ya serikali kwa vurugu kwa lengo laku weka kiongozi tofauti madarakani. Kikao hicho ndani ya mahakama yenye ulinzi mkubwa mjini Stuttgart, itakuwa ni mwanzo wa kusikizwa kwa kesi tatu mfululizo za watu 27 kwa ujumla, ambao wame shutumiwa kwa kupanga njama iliyo vunjwa na mamlaka mwisho wa 2022. Wanachama teisa wa kundi la Reichsbuerger ((tafsiri yake ikiwa ni raia wa Reich)) watalengwa katika kesi hiyo, tisa hao wametuhumiwa kupanga njama yakuweka sheria kali yakijeshi baada yakufanya mageuzi hayo ya serikali. ((Katika mwaka wa 2016, mashirika yakijasusi ya ujerumani yalikaridia uwepo wa takriban wanachama 21,000 wa Reichsbuergers, ambao hawaitambui Ujerumani ya sasa kama taifa halali.))

Watu karibu 80 wamepoteza maisha baada ya kusombwa na maji ya mafuriko nchini Kenya, kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha hasa katika jiji kuu Nairobi. Naibu rais Rigathi Gachagua, amewatembelea baadhi ya watu walioathiriwa na mafuriko jijini Nairobi, na kuwataka raia wa nchi hiyo kuachana na tabia zinazohatarisha maisha yao, kipindi hiki cha mvua. Mbali na Kenya, Tanzania pia imeshuhudia changamoto hii ya mafuriko, ambapo serikali imesema, watu zaidi ya 150 wamepoteza maisha, huku mitaa kadhaa ikijaa maji hasa jijini Dar es salaam. Mji wa Kalemie nchini DRC na baadhi ya maeneo nchini Burundi pia yanaendelea kushudia mafuriko makubwa.

Viongozi wa dunia na makundi ya misaada wanaonya uvamizi wa Israel katika mji wa kusini wa Rafah utasababisha machafuko. Juhudi za kidiplomasia ziliongezeka leo Jumapili kufikia makubaliano ya muda mrefu ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza, wakati Israel ikifanya mashambulizi zaidi ya anga na makombora katika eneo hilo lililoharibiwa na vita. Video mpya ya mateka wawili wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas tangu shambulizi la Oktoba 7 la kundi hilo lilichochea ghadhabu mpya nchini Israel, ambako waandamanaji wamezidisha shinikizo kwa serikali kufikia makubaliano.

Katika soka mwalimu wa Atletico de Madrid amesema matusi yaubaguzi wa rangi dhidi ya mpinzani wao katika ushindi wa goli tatu kwa moja dhidi ya Athletic Bilbao, ni swala lakijamii Uhispani, si tu kwa mashabiki wa timu ya Atletico. Nico Williams alimuomba mwamuzi wa mechi asimamishe mechi katikakati ya kipindi cha kwanza, baada yakulengwa na sehemu ya mashabiki wa nyumbani ambao walikuwa wakimzomea kwa kelele za nyani alipokuwa akijaribu kupiga mpira. Williams alifunga goli lakusawazisha kabla ya mwisho wa kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, ila Atletico ilishinda mechi hiyo baada yakufunga goli zingine mbili katika kipindi cha pili nakumaliza mechi hiyo kwa ushindi wa goli tatu kwa moja.

Share