Taarifa ya Habari 3 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema waendesha mashtaka wa shirikisho walifanya uamuzi mubaya kuruhusu dhamana kwa mfungwa wa uhamiaji, ambaye baadae anadaiwa kumshambulia bibi mmoja mjini Perth katika tukio la uvamizi wa nyumba.


Waziri Mkuu Anthony Albanese ame ahidi serikali ya shirikisho ita ongeza juhudi kushughulikia visa vya ukatili wa nyumbani. Mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri washirikisho namajimbo, ume sababisha tangazo la mpango, unao jumuisha $925.2milioni kuanzisha mradi wakuondoka katika vurugu kwa muda wakudumu, ulio wasilishwa na serikali ya Morrison pamoja na hatua zingine za usalama wa mtandaoni kama, marufuku kwa picha feki za ngono, pamoja na kinacho julikana kama doxxing [[uvujaji wa taarifa za kibinafsi kwa makusudi bila ridhaa]].

Walipa kodi kote jimboni Queensland wanatarajiwa kupata afueni baada ya serikali ya jimbo kutangaza jeki ya $2.5 bilioni kupunguza gharama ya shinikizo za maisha. Uwekezaji huo utasaidia familia kote jimboni kupokea punguzo ya $1,000 kwa bili zao za umeme. Kiongozi wa jimbo hilo Steven Miles alifanya tangazo hilo kwa kile ambacho kitakuwa gharama kubwa zaidi ya mpango wa maisha ya serikali yoyote ya jimbo.

Soko kubwa la chakula Woolworths limeripoti ongezeko dogo katika mauzo yake ya chakula ya nyumbani katika robo iliyopita baada ya kupungua kwa bei. Soko hilo limesema mauzo ya vyakula nchini Australia yalionesha ongezeko la asilimia 1.5 kwa $12.6 bilioni, wakati wastan ya bei ikishukwa kwa asilimia 0.2. Kwa ujumla, soko la Woolworths limeripoti ongezeko ya asilimia 2.8 ya faida katika mtandao wayo wote, unao jumuisha soko zake za New Zealand pamoja na maduka ya Big W.

Umoja wa Mataifa unakisia kwamba itagharimu hadi dola bilioni 40 na miaka 16 kuweza kuurejesha Ukanda wa Gaza kwenye hali ya kawaida baada ya uharibifu mkubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu Vita vya Pili vya Dunia. Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Abdallah al-Dardari, alisema siku ya Alkhamis (Mei 2) kwamba makisio ya awali ya Mfuko Maendeleo wa Umoja huo yalikuwa yanaonesha kwamba ujezi mpya wa Gaza utapindukia dola bilioni 30 na kwamba unaweza kufikia hadi dola bilioni 40.

Njaa na Utapiamlo unaenea kote nchini Sudan, mwaka moja tangu kuzuka kwa vita kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha dharura cha (RSF) huku ikiwa hakuna dalili ya vita kusitishwa hivi karibuni. Katika baadhi ya kambi za watu waliokoseshwa makaazi huko Darfur Kaskazini, wakaazi, madaktari na wafanyakazi wa misaada wanasema watu wamelazimika kula udongo na majani.

Kenya na Tanzania zinajiandaa kuwasili kwa kimbunga Hidaya siku ya Alhamisi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Afrika Mashariki na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 350 na maelfu ya wengine kuyakimbia makazi yao.
Mafuriko ambayo tayari yamegharimu maisha ya zaidi ya watu 188 nchini Kenya tangu mwezi Machi pia yamesababisha watu 165,000 kuyahama makazi yao na 90 hawajulikani walipo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema. Serikali imewataka wananchi kuendelea kuwa waangalifu.

Share