Taarifa ya Habari 5 Julai 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema muda ambao Seneta Fatima Payman amefanya tangazo lake lakujiuzulu kutoka chama cha Labor ni swala linalo mhusu.


Wiki moja baada ya Seneta huyo kusimamishwa uanachama kwa muda usiojulikana kwa kuvuka sakafu kupigia kura uhuru wa utaifa wa Palestina, Bi Payman alifanya uamuzi huo jana Alhamisi 4 Julai, kuondoka katika chama kilicho mkaribisha katika siasa. Bi Payman amesema amefanya uamuzi wakuondoka katika chama hicho naku keti na wabune huru jana asubui, baada yakuzingatia maoni ya Bw Albanese wakati wa maswali na majibu Jumatano kuwa alimtarajia kufanya tangazo kuhusu hatma yake.

Wanasiasa wa shirikisho wame wakosoa vikali waandamanaji walio panda juu ya bunge la taifa jana Alhamisi 4 Julai nakufunga mabango yanayo ishtumu serikali ya Australia kwa kushiriki katika uhalifu wakivita na mauaji ya kimbari Gaza. Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema waandamanaji wanao unga mkono Palestina, wanastahili hisi uzito wa sheria akisema matendo yao yalikandamiza demokrasia. Polisi wa A-C-T wame wakamata wanaume watatu na mwanamke mmoja, wanao tarajiwa kufunguliwa mashtaka ya makosa ya uasi wa shirikisho. Kundi la wanaharakati kwa jina la Renegade Activists, limedai uwajibikaji wa maandamano hayo, baada yakuondoka katika paa la bunge baada ya masaa kadhaa.

Ofisi wa ushuru ya Australia inajiunga na soko la uhalifu wakifedha la Australia. Shirika hilo huru lisilo la faida husaidia kuratibu shughuli za akili na kuchangia data katika sekta za umma na binafsi, kuchunguza nakuzuia uhalifu wakifedha na mtandao. Stephen Jones ni Waziri wa huduma za fedha, amesema maendeleo hayo yanata saidia uchunguzi kuchangiwa kwa hatua za haraka na utapeli.

Utabiri baada ya kura kupigwa nchini Uingereza unaonesha kuwa chama cha Labour kimeibuka na ushindi wa kishindo, huku kiongozi wake, Keir Starmer akielekea kuchukuwa nafasi ya Rishi Sunak kama waziri mkuu mpya. Matokeo yaliyopitiwa na mashirika mbalimbali ya habari yanaashiria kuwa chama cha Labour kinachofuata siasa za mrengo wa kati kushoto kimepata viti 410 kati ya 650 bungeni, huku wahafidhina wa mrengo wa kulia, Conservative, wakimudu kukusanya viti 131 tu, kiwango cha chini kabisa kwa chama hicho kwa zaidi ya miaka 100 sasa.

Takriban watu 25 wamefariki wakati boti lao lilipozama walipokuwa wakijaribu kukimbia mapigano kati ya vikosi vya wanamgambo vya RSF na jeshi la serikali kusini mashariki mwa Sudan, kundi linalounga mkono demokrasia limesema siku ya Alhamisi. Janga hili jipya linakuja wakati ambapo wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (FSR), katika vita dhidi ya jeshi, wamepata mafanikio makubwa tangu mwisho wa mwezi wa Juni katika eneo hili kubwa la Sudan, linalokabiliwa na mapigano makali.

Muongo mmoja baada ya janga la Ebola ambalo limeua zaidi ya watu 11,000 nchini Sierra Leone hivi sasa inakabiliwa na homa mbaya inayosababisha kifo inayoitwa Lassa. Virusi vinaambukizwa kwa njia ya binadamu kupitia panya ambao wanaugua. Sierra Leone tangu haijarekodi kesi za ebola tangu mlipuko ulipomalizika mwaka 2016, shukran kwa kiasi kutokana na chanjo. Wilaya ya Kenema, ambacho ni kituo kikuu cha Ebola, wanasayansi wanatumia mafunzo waliyopata muongo mmoja uliopita kujaribu kusitisha kusambaa kwa homa ya Lassa. Kwa ujumla kiwango cha vifo ni asilimia moja, Lassa haijakaribia kuwa ni ya kutisha kama Ebola, ambayo iliua takriban asilimia 50 ya wagonjwa, kwa mujibu wa shirika la afya duniani.

Share