Taarifa ya Habari 7 Mei 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali imesema ita kuwa na akiba ya bilioni moja ya dola katika bajeti ya shirikisho ijayo, kwa kukata matumizi ya huduma ya umma ya wakandarasi, washauri na wafanyakazi wengine wa nje.


Chama cha Greens kimesema msaada wa wanafunzi ambao hufanya kazi ya lazima haifanyi yakutosha kushughulikia shinikizo la haraka la gharama ya maisha. Serikali ya shirikisho imetangaza itatoa malipo ya $320 (($319.50)) kila wiki kwa maelfu ya wanafunzi wa ualimu, wauguzi na wafanyakazi wa jamii, ambao hufanyakazi bila kulipwa kama sehemu ya shahada yao. Malipo hayo ambayo ni nyongeza ya msaada wa mapato ambayo wanaweza kuwa wakipokea tayari, ita anza kutumiwa kuanzia July 2025 na kufaidi takriban wanafunzi elfu 68 wa vyuo pamoja na wanafunzi elfu tano wa elimu ya ufundi na mafunzo.

Jumuiya yawa Islamu ya Magharibi Australia, imeomba hatua za ziada zichukuliwe kutokomeza unyanyapaa unao zingira swala la afya ya akili, pamoja na utoaji wa rasilimali kwa matibabu na utambuzi. Wito huo umejiri baada ya kifo cha mvulana wa miaka 16, aliye kuwa mwanafunzi wa shule ya upili aliye pigwa risasi hadi kufa na polisi, baada yakumdunga mwanaume mmoja kisu mgongoni katika sehemu yakuegeza magari ya duka katika kitongoji cha Willeton jioni ya Jumamosi ((Mei 4)). Wazazi wa mvulana huyo awali walikuwa wame elezea polisi wasiwasi wao kuhusu itakadi kali alizo kuwa amepata kutoka mitandao yakijamii.

Kenya, Uganda, Rwanda, DRC na Sudan Kusini zimeamua kuweka nguvu ya pamoja kufanikisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi SGR inayopita Afrika Mashariki. Mawaziri wa uchukuzi kutoka mataifa hayo wamekubaliana kwa pamoja kutafuta wafadhili na wajenzi wa reli hiyo, kurekebisha mkataba wa maelewano na kuhusisha mataifa ya DRC na Sudan Kusini na vile vile jinsi ya kugawana majukumu ya kulinda reli hiyo ya SGR. Mwaka 2014 mataifa ya Kenya Rwanda na Uganda yaliweka makubaliano kujenga reli ya SGR kutoka Mombasa , Kampala mpaka Kigali Rwanda lakini ujenzi huo alisimamishwa ghafla mfadhili mkuu China ilipokukataa kuendelea kuufadhili baada ya kukosa maelewano na Uganda.

Kundi la Hamas ilimetangaza siku ya Jumatatu, Mei 6, 2024, kwamba limekubali pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na wapatanishi, Misri na Qatar, kwa Ukanda wa Gaza. Afisa wa Israel anasema pendekezo la kusitisha mapigano lililoidhinishwa na Hamas halikubaliki kwa Israel, linaripoti shirika la habari la REUTERS. Israel ilikuwa haijatoa msimamo wake, ambapo jeshi lake Jumatatu lilisema watu katika maeneo ya mashariki mwa mji wa Rafah wanapaswa kuelekea kwenye eneo ambalo jeshi limeliita eneo kubwa la kibinadamu ambalo linajumuisha Khan Younis, katika hatua ambayo inajiri kabla ya shambulizi lililopangwa la Israel huko Rafah.

Jeshi la kikanda la jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC likishirikiana na Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika msako wa waasi wa M23 na washirika wao. Vikosi hivyo vimetangaza kufanya operesheni za kuwadhibiti waasi hao ili kulinda amani na usalama na kulinda raia na mali zao dhidi ya vitisho. Tangazo hili linakuja baada ya mashambulizi ya bomu yaliyotokea tarehe 03 Mei katika kambi za watu waliofurushwa makwao kwenye eneo la magharibi mwa mji wa Goma, ambayo yalisababisha vifo vya watu 16 na kujeruhi watu 35.




Share