Taarifa ya Habari 9 Julai 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Wakaaji wa Alice Springs wame amka baada ya usiku wa kwanza wa amri ya kuto toka nje ambayo ili wekwa kwa ajili yakupunguza uhalifu.


Amri hiyo ya kuto toka nje kwa siku tatu, inayo tumiwa na jeshi la polisi inatumiwa kwa kila mtu na jiografia, na katikati ya mji kati ya saa nne asubhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Amri hiyo ime anzishwa baada ya wimbi la uhalifu wikendi iliyo pita, iliyo jumuisha tukio la watu themanini walio pigana.

Mashirika ya walemavu yana wasiwasi mpango wa serikali wakupiga marufuku huduma za kujamiana katika mfumo wakitaifa wa bima ya ulemavu, uta athiri haki za binadam za wanao tumia mfumo wa N-D-I-S. Sheria za sasa za NDIS zinaruhusu watumiaji kudai huduma zakujamiana kama sehemu ya bajeti yao binafsi, ambayo waziri wa NDIS Bill Shorten anapanga kubadilisha kama sehemu ya mageuzi mapana. Serikali ilifeli kupitisha muswada wayo wa NDIS kabla ya mapumziko ya majira ya baridi, baada ya upinzani wa Mseto na chama cha Greens kutuma muswada huo katika kamati ya seneti.

Mwanaume mmoja ame kamatwa baada ya mwanamke kudungwa kisu nakufa katika nyumba moja, katika eneo la Magharibi Sydney katika tukio linalo tuhumiwa kuwa ni mauaji ya unyanyasaji wa nyumbani. Polisi na wahudumu afya wali itwa katika nyumba hiyo ambayo iko katika barabara ya Great Western Highway mchana wa Jumatatu 8 Julai, ambako walimpata mwanamke aliye kuwa na majeraha mabaya kifuani. Mwanamke huyo mwenye miaka 21, alitibiwa katika eneo la tukio ila hakuweza okolewa. Polisi walizindua msako wa mwanaume huyo mwenye miaka 22 aliye onekana aki kimbia kutoka sehemu ya tukio, akivaa kote nyeusi, suruali nyeusi na shati ya mchezo wa vikapu ya rangi nyekundi na nyeusi.

Mahakama ya kijeshi katika eneo tete la mashariki mwa DRC imewahukumu adhabu ya kifo wanajeshi 22 leo Jumatatu kwa “kumkimbia adui” wakati wa mapigano na waasi wa M23, mwanasheria mmoja ameliambia shirika la habari la AFP. Wanajeshi 16 walihukumiwa kifo katika kesi moja kwenye jimbo la Kivu Kaskazini, na wengine sita katika kesi tofauti, siku chache baada ya wanajeshi 25 kupewa hukumu kama hiyo. Hukumu hiyo ya hivi karibuni imekuja wakati waasi wa M23, ambao Kinshasha inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono, wiki iliyopita waliiteka ardhi mpya katika eneo la kaskazini lenye mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka miwili na nusu katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Madaktari nchini Kenya Jumatatu wamefanya maandamano jijini Nairobi na kuweka kambi katika Wizara ya Afya ili kuishinikiza serikali kuwaajiri madaktari wanafunzi katika vituo vya afya na kuwalipa mshahara kwa mujibu wa mkataba wa pamoja wa maafikiano wa mwaka 2017. Mwezi Mei, baada ya siku 56 za mahangaiko makubwa katika hospitali za umma nchini humo, kufuatia mgomo wa madaktari, pande mbili kwenye mazungumzo hayo zilieleza kuwa zimefikia muafaka uliowezesha kutiwa saini mkataba wa kurejea kazini mara moja kama njia ya kipekee ya serikali kujitolea kutimiza utekelezaji kamili wa mkataba huo wa pamoja wa maafikiano wa mwaka 2017.

Rwanda imesema Jumatatu kwamba inafahamu nia ya Uingereza ya kusitisha mpango wake wa kuwahamishia wahamiaji katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Katika taarifa, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, amesema Rwanda inazingatia nia ya serikali ya Uingereza kusitisha Mkataba wa Ushirikiano wa Uhamiaji na Maendeleo ya Kiuchumi, uliopitishwa na mabunge ya nchi hizo mbili. Taarifa hiyo pia imesema ushirikiano huo ulianzishwa na serikali ya Uingereza ili kushughulikia mgogoro wa uhamiaji usio wa kawaida unaoiathiri nchi hiyo na kwamba ni tatizo la Uingereza na sio Rwanda.

Share