Taarifa ya Habari 9 Mei 2024

City - Swahili.jpg

Serikali ya Australia ita imarisha miradi ya gesi katika hatua yakutoa suluhu kwa ongezeko la mahitaji pamoja nakusaidia mchakato wakuhamia kwa uzalishaji sufuri kufikia 2050, hoja ambayo imefichua kuwa uchimbaji utaendelea zaidi ya tarehe hiyo.


Tangazo hilo limejiri licha ya wito wakimataifa waku punguza matumizi ya mafuta wakati wa ongezeko la joto katika mazingira, wakati shirika la nishati la dunia lina toa hamasa kwa mapungozo makubwa ya matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi kwa ajili yakufikia malengo yakimataifa ya mazingira.
Alipo tangaza mkakati wa usoni wa gesi ya Australia, Waziri wa Rasilimali na Kaskazini Australia Madeleine King, amesema gesi itakuwa muhimu kwa utoaji wa 82% ya nishati mbadala kufikia 2030.

China ime ishtumu Australia kwa upepelezi nakudai hiyo ndiyo sababu ya tukio ambako moto uli dondoshwa mbele ya helicopta ya jeshi la wanamaji wa Australia, naku ilazimisha kuchukua hatua yaku kwepa. Australia imesema tukio hilo halikuwa salama na kinyume cha taaluma, wakati China imetupilia mbali madai hayo. Naibu waziri wa Ulinzi, Matt Thistlethwaite ali eleza makala ya News Breakfast, ya shirika la habari la ABC kwamba, serikali imekuwa ikifanya kazi kuimairisha tena uhusiano wayo na China.

Victoria Police inajiandaa kuomba radhi kwa nafasi yake katika vizazi vilivyo ibiwa kama sehemu ya mageuzi kutoka kwa uchunguzi wakusema ukweli wa jimbo hilo. Kamishna Mkuu Shane Patton amethibitisha ahadi ya jeshi la polisi la jimbo hilo, ita jumuisha michakato ya jinsi wa Aboriginal wanaweza kabiliana na polisi. Michakato hiyo itajumuisha kupanuliwa kwa mafunzo ya uelewa wakitamaduni, katika shirika hilo pamoja nakuboreshwa kwa ripoti za takwimu za polisi kuhusu wa Aboriginal. Kwa ujumla, Victoria Police itafanya mageuzi 79 kufikia mwisho wa 2025 kama sehemu ya jibu lake kwa tume ya hakimu Yoorrook.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alielezea kuwa ni uhaini kwa hatua ya tangazo la kampeni la chama cha upinzani ambalo linaonyesha bendera ya taifa inayowaka moto, huku uhasama kati ya vyama vya siasa ukiongezeka wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu. Tangazo la kampeni lililotolewa siku ya Jumatatu na chama cha Democratic Alliance linatumia bendera inayowaka kama alama ya kile inachosema ni hatari kubwa ya chama tawala cha African National Congress kubakia madarakani katika muungano na vyama vya mrengo wa kushoto. "Nadhani ni uhaini," Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika jimbo la Limpopo. "Ni kitendo cha kisiasa kibaya zaidi ambacho mtu yeyote anaweza kukitekeleza," alisema, akishutumu DA kwa kunajisi ishara ya umoja wa kitaifa.

Mgomo wa siku 56 wa madaktari katika hospitali za umma nchini Kenya, hatimaye wafikia muafaka, baada ya kufanya makubaliano na serikali siku ya Jumatano, na kutia saini mkataba wa kurejea kazini mara moja licha ya kutofikia muafaka kuhusiana na mishahara ya madaktari wanafunzi.
Muungano wa Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno KMPDU ambao unawakilisha zaidi ya madaktari 7,000, umetangaza kufikia muafaka katika utekelezaji kamili wa mkataba wa pamoja wa maafikiano wa mwaka 2017. Na hivyo kuumaliza mgomo huo baada makubaliano yaliyotiwa saini kwenye ukumbi wa Jumba la Kimataifa la Mikutano la Kenyatta, KICC, jijini Nairobi. Katibu mkuu wa chama cha madaktari KMPDU, Dkt Davji Atellah, amesema kuwa kutiwa saini mkataba wa kurejea kazini mara moja ni njia pekee ya serikali katika kutekeleza kikamilifu mkataba huo wa pamoja wa maafikiano wa mwaka 2017 unaojumuisha masuala mbalimbali yakiwemo uajiri na ulipaji wa mshahara wa kila mwezi kwa madaktari wanafunzi.

Katika michezo, Mwalimu Jo Yapp ametangaza timu yake ya kwanza ya Wallaroos, itakayo pambana na timu ya raga ya wanawake ya Canada, katika mechi yakufungua michuano ya Pacific Four mjini Sydney. Mchezaji huyo wa zamani wa England aliye chukua mikoba yakuwa mwalimu wa taifa wa timu ya wanawake ya Australia mwaka jana, ame jumuisha mchezaji wa ACT Brumbies Sally Fuesaina na wachezaji wawili kutoka Western Force, Hera-Barb Malcolm Heke na Samantha Wood ambao watakuwa wachezaji wa ziada katika mechi itakayo chezwa Jumamosi katika uwanja wa Allianz. Wachezaji Malcolm Heke na Wood walionesha umahiri wao msimu huu walipo chezea Western Force katika mechi za Super Rugby Women mwaka huu, wakati Fuesaina anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa katika umri wa miaka 32. Yapp ametangaza kikosi chenye uzoefu mkubwa sana, kitakacho pambana na timu namba 4 kwa ubora duniani katika raga ya wanawake.

Share