Uchunguzi wa Seneti waunga mkono mswada tata wa uhamisho

Minster for Social Services Amanda Rishworth

Minster for Social Services Amanda Rishworth Source: AAP

Uchunguzi wa Seneti umependekeza serikali ipitishe mswado wake wenye utata, utakao fanya iwe rahisi kuwafukuza nchini walio ndani ya vizuizi vya uhamiaji.


Muswada huo utaipa serikali mamlaka yakuweka marufuku kwa watu kutoka nchi ambazo, serikali zao zinakataa kuwapokea raia wanao rudishwa.

Kamati ya bunge imependekeza serikali ipitishe muswda tata, unao watishia watu ambao si raia na kifungo gerezani, kama hawata shirikiana na amri yakuondoloewa nchini.

Mswada huo unaipa serikali mamlaka yaku walazimisha wafungwa wa uhamiaji, kutii amri yakuondolewa kwao Australia, na wanao kataa kutii amri hiyo wata kabiliwa kwa kifungo cha takriban miezi 12 gerezani.

Pendekezo lingine la pekee ilikuwa kwamba Waziri azingatie, madhara kwa jamii anapo taja nchi kama nchi yenye wasiwasi yakurejesha mtu, mamlaka hayo yana mruhusu waziri husika kuweka marufuku pana, kwa utoaji wa viza kwa watu kutoka mataifa ambayo serikali zao zinakataaa kuwapokea raia wao ambao wamefukuzwa nchini.

Share