Viongozi wadini, Waziri Mkuu waomba uwepo wa heshima na maelewano katika jamii

Australia Church Stabbing

A damaged car sits parked outside the Christ the Good Shepherd church in suburban Wakely in western Sydney, Australia, Tuesday, April 16, 2024. Australian police say a knife attack in Sydney that wounded a bishop and a priest during a church service as horrified worshippers watched online and in person, and sparked a riot was an act of terrorism. (AP Photo/Mark Baker) Source: AAP / Mark Baker/AP

Viongozi kutoka jumuiya za wayahudi, waislamu na wakristo mjini Sydney wame kemea kwa pamoja vurugu na maneno yakugawanya ambayo yame ibuka kufuatia matukio mawili ya shambulizi ya visu mjini Sydney.


Viongozi hao wana ongezeza sauti zao kwa wito wa waziri mkuu wa kuwepo kwa maelewano ya jamii na kukuza ushirikishwaji. Viongozi wakidini wamesema baadhi ya majibu kwa uhalifu wa matumizi ya visu mjini Sydney, unadhoufisha mshikamano wa kijamii wa Australia.

Makundi yawa yahudi, waislamu na wakristo yametoa taarifa kuhusu mivutano ya hivi karibuni pamoja na vurugu mjini Sydney. Hali hiyo imefuata kile ambacho polisi na mashirika ya ulinzi yame ita shambulizi lakigaidi katika kanisa la Christ The Good Shepherd Church ambalo liko katika kitongoji cha Wakeley.

Wakati taarifa na video za shambulizi hilo zilikuwa zinasambaa katika mitandao yakijamii, ma mia ya watu walifika katika kanisa hilo waki dai mshambuliaji huyo aletwe nje ili wamshughulikie.

Muda mfupi baadae makabiliano yali zuka kati ya polisi na watu walio kuwa nje ya kanisa, ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi walijeruhiwa pamoja na magari ya polisi kuharibiwa.

Share